Kanuni kwa Maendeleo ya Kidijiti


Usukumwe na Data

  • - Andaa programu ambayo matokeo yanaweza kupimwa kwa mwendelezo.
  • - Tumia kwa mafanikio data zilizopo, ikiwa ni pamoja na kufungua seti za data na pamoja na mifumo yenye uwezo wa kufanya kazi kwa kuingiliana.
  • - Tumia njia nzuri za kukusanyia data.
  • - Saidia upungufu wa uelewa wa karibu kwa kuchangia data katika maendeleo ya jamii.
  • - Tumia data zenye ubora au data zinazokwenda na wakati kusaidia uamuzi wa haraka, kuboresha uandaajii wa programu kwa ajili ya watumiaji na mkakati wa kutoa taarifa.
  • - Wasilisha data katika mifumo ambayo ni rahisi kuitafsiri na kuifanyia kazi, kama vile ubainishaji wa data.
  • - Anzisha utamaduni wa kutumia data kwa kuweka kipaumbele katika kujenga uwezo na jitihada za kutumia data.
  • - Jenga imani kuhusu ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Kusanya data kutoka vyanzo mbalimbali.
  • - Bainisha na kutumia data za wazi na viwango vyenye uwezo wa kufanya kazi kwa kuingiliana.
  • - Kusanya na kutumia data zinapofaa kulingana na kanuni na viwango vya kimataifa.