Kanuni kwa Maendeleo ya Kidijiti


Tumia viwango vya wazi, Data za Wazi, Vyanzo Huru na Ubunifu wa wazi

  • - Tafsiri na eleza nini maana ya kuwa wazi katika jitihada zako.
  • - Tumia na panua viwango huru vilivyopo - uwazi umewekwa, kukubalika, kufuatwa na kuendelezwa na jamiii ambayo inawezesha ushirikishaji wa data zilizomo katika nyenzo na mifumo.
  • - Shirikisha Data ambazo sio nyeti baada ya kuhakikisha mahitaji ya usiri wa data yameshughulikiwa bila vizuizi katika matumizi ya data ili kuwezesha ubunifu huru kwa kundi au sekta yoyote.
  • - Tumia majukwaa ya wazi yaliyopo pale inapowezekana kusaidia ushirikishaji wa data, kuunganisha mfumo au nyenzo zako pamoja na wengine na kuongeza uwezo wa kukubali mabadiliko ili kutumika kwa mahitaji ya siku zijazo.
  • - Wekeza katika programu kwa manufaa ya umma.
  • - Anzisha msimbo mpya kuwa chanzo huru ambacho mtu yeyote anaweza kuona, kunakili, kurekebisha na kushirikishana na shirikisha msimbo mahali pa umma pa kuhifadhia.
  • - Wezesha ubunifu kwa kushirikishana bure bila vizuizi, kushirikiana kwa upana na kuunda kwa pamoja ufumbuzi iwapo unaleta maana katika mazingira yako.