Kanuni kwa Maendeleo ya Kidijiti


Zingatia Usiri na Usalama

  • - Fafanua umiliki wa data, uhuru na ufikiaji kabla ya data yoyote kukusanywa/kuchukuliwa. Amua ni sheria na kanuni zipi zinahitaji kufuatwa.
  • - Endeleza matakwa mazuri ya watumiaji wa mwisho na wale ambao data zao zilikusanywa awali kwa ajili ya mipango yako kwa uungaji mkono usiri wa mtumiaji na kuhakikisha usalama wa data na utekelezaji wa mradi kimaadili.
  • - Fanya uchanganuzi wa faida/hatari ya data zitakazochakatwa, ikijumuisha nani atakayepata faida na nani atakayekuwa hatarini.
  • - Tathmini hatari ya ufikiaji usioruhusiwa au kutoka kimakosa kwa data zilizohifadhiwa. Kuelewa kwamba hatari imezingatiwa kulingana na mazingira, siyo tu kwa nchi lakini pia kwa jumuiya, watu na kwa kipindi maalumu.
  • - Punguza ukusanyaji wa taarifa binafsi zinazombainisha mtu. Zingatia umuhimu wa taarifa binafsi za mtu katika mafanikio na madhara yayakayotokea kama data hizo zitawekwa wazi kwa mtu wa tatu.
  • - Bainisha na kufuatilia taarifa zozote binafsi na nyeti zilizokusanywa wakati wote wa mradi: Andaa mpango wa uharibifu au ulinzi wa utunzaji wa nje ya mfumo wa data nyeti katikati na mwishoni mwa mradi.
  • - Uwe wazi kwa watu ambao data zao zimekusanywa kwa kuwaeleza jinsi mradi wako utakavyozitumia na kuzilinda data zao.
  • - Pata ridhaa inayotolewa baada ya kupata taarifa kabla ya kukusanya data. Ni muhimu kuhakikisha kwamba washiriki wanaelewa kwa nini data zao zimekusanywa, data hizo zinatumikaje na zinashirikishwaje, wanawezaje kuzifikia au kuzibadilisha data zilizokusanywa na kwamba watapewa uchaguzi wa kukataa kushiriki.
  • - Linda data kwa kufuata utendaji mzuri kwa ajili ya kulinda na kuzuia ufikiaji wa data.