Kanuni kwa Maendeleo ya Kidijiti


Shirikiana

  • - Elewa namna kazi yako inavyoendana na mandhari ya maendelo ya ulimwengu. Wabainishe wengine wanaoshughulikia tatizo kama lako katika mazingira mengine ya kijiografia na kama kuna jumuiya yenye suala kama hilo.
  • - Shirikisha wataalamu anuwai wa taaluma mbalimbali, nchi na tasnia katika muda wote wa mradi.
  • - Panga kushirikiana kuanzia mwanzoni. Andaa shughuli za ushirikiano katika mapendekezo, mpangokazi, bajeti na mchanganuo wa kazi. Bainisha viashirio kwa ajili ya upimaji wa ushirikiano katika mpango wako wa ufuatiliaji na tathmini.
  • - Tunza kumbukumbu za kazi, matokeo, mchakato na utendaji mzuri. Shirikisha msimbo wako katika jumuiya ya chanzo huru, chapisha nyaraka chini ya Leseni ya Haki ya Ubunifu na utendaji kwa kushiriki katika mikutano na majukwaa mengine ya kushirikisha uzoefu wako uliojifunza na kujifunza kutoka kwa wataalamu wengine.
  • - Fafanua namna mradi wako utakavyochangia maendeleo ndani ya nchi. Ushirikiano ni hatua ya kwanza ya ubadilishanaji na uchukuaji taarifa – fafanua jinsi kazi yako inavyoweza kuunganishwa na mifumo ya ndani na viwango gani unavyovihitaji kufuata kwa ajili ya kuwezesha uunganishwaji huu.